0
Msanii kutoka Tip Top Connection ya Manzese, Khaleed “Tunda man” Ramadhan amefunguka kwa kusema kuwa Tip Top ya kipindi cha nyuma haikuwa na majungu.
Akizungumza na The Jump off ya Times FM, mkali huyo wa “Msambinungwa” amekiri kuwa Tip Top ya miaka ya nyuma ilikuwa iko vizuri zaidi ya sasa.

“Nakubaliana na wewe Tip Top ya enzi zile za tunapanda ilikuwa kama timu ya taifa vile, maana umoja ulikuwepo na wala hakukuwa na majungu yani kila mmoja alisimamia nafasi yake” alisema Tunda.

Pia Tunda Man alisema anatamani Cassim Mganga arudi tena kundini Tip Top kutokana na uwezo wake pamoja na sauti yake.

“Kiukweli Cassim natamani arudi yani kwakuwa bado hatujampata mbadala wake, unajua sauti yangu na yake(Cassim) zilikuwa zinaendana sana na Madee akipita na bass basi inakuwa poa sana, kwa kweli hakuna aliyeziba pengo lake” alimaliza

Tunda ameenda mbali zaidi kwa kusema baada ya kuondoka kwa Cassim Mganga, Tip Top imeyumba.

Post a Comment

 
Top