0
Baraza la sanaa Tanzania, BASATA wameufungia rasmi wimbo wa Roma Mkatoliki uitwao ‘Viva Roma Viva’.

Hatua hiyo imezikumba na nyimbo nyingine pia zenye ujumbe kama uliopo kwenye wimbo huo.

BASATA wamesema sababu kubwa ya kuufungia wimbo huo wa Roma ni kwamba hakuna ushahidi wa vitu vilivyoimbwa katika wimbo huo.

Baada ya taarifa za kufungiwa kwa wimbo huo, Roma alitumia Instagram kupost screenshot ya taarifa hiyo na kuandika;

“Life is Not Fair!!!!!! TUNAKUFA MASIKINI KWA KUWATETEA WANYANG’ANYI!!!!!!!!!! Eee Mungu
Baba Wa Mbinguni
Nisaidie!!! #Democracy
#Politics
#Justice
#Freedom

#ViVaROMAViVa
#ViVaROMAViVa
#ViVaROMAViVa”

Saa chache baada ya wimbo huo kutoka Septemba 9, 2015 rapper huyo alitumia Instagram yake kuandika kuwa ametishiwa kufungiwa wimbo wake.

“Wanataka kuifungia nyimbo yangu!! Kisa tu nimeongea ukweli!! Inaniuma sana natamani hata kulia nikiona ukweli haupewi nafasi!! Niombeeni na mnikumbuke kwenye sala zenu ndugu zangu!! Viva Roma Viva”.

Post a Comment

 
Top