0

Kama umetazama vizuri video ya msanii Galatone “Sina Mali” kuna neno Kapasta 4 Real Project, Kapasta 4 Real Project ni kama lebo ambayo inasimamia kazi za wasanii ambao wapo kwenye

Project hiyo chini ya usimamizi wa Producer Kapasta 4 Real.

Akipiga stori na Ergon Elly kupitia 97 Show ya 97.1Mhz Njombe Tanzania,Producer Kapasta 4 Real amesema kuwa anasimama kwa muda ku-produce muziki na kujikita zaidi kwenye usimamizi wa wasanii kwani ana amini kuwa kusimamia project zake kunalipa zaidi kuliko kukaa studio na kutengeneza muziki.


Wakati huo huo amezungumzia ujio mpya wa Galatone ambapo Januari au Februari 2016 wataachia wimbo mpya “SAMAKI” ambao sasa hivi unaandaliwa studio na producers tofauti.


Sikiliza full Interview hapa….

Post a Comment

 
Top