Tetemesha Entertainment inamtambulisha msanii mpya kutoka
Rock City, aitwaye - COYO. Huyu atakuwa ndio msanii wa kwanza anaye Rap kufanya
kazi na Tetemesha baada ya Hussein Machozi, Sajna na Barakah Da Prince.
NOMA, ndio jina la wimbo rasmi unaomtambulisha COYO ambao
umerekodiwa jijini Mwanza chini ya
producer mkali na mwenye dalili za kuja kusumbua kwa kazi kali aitwaye Day
Dream.
Moja ya utambulisho ambao COYO alioamua kuutumia katika kazi zake,
ni pamoja na kuchanganya maneno ya Kisukuma kwenye nyimbo zake.
“Nimeamua kuchanganya Kisukuma kwenye wimbo wangu maana mimi
ni msukuma, na pia napenda kuonesha uzalendo kuanzia kwenye utunzi kama
Mtanzania halisi ninaye jivunia asili yangu, na pia nataka iwe moja ya
utambulisho wangu wa kunitofautisha na wengine” amesema COYO .
Hii ni baadhi ya mistari aliyochanganya na Kisukuma pamoja
na tafsiri zake:
“Pesa Shane shone (pesa zangu
zote )/
Nakwine unine nami
npone (nikupe unipe na mi nipone )/
Nyonga mpaka nikome /
Nakutoole (nikuoe)/
Nkutwale(nikupeleke)/
Kokaya kome (nyumbani kome )/”
Licha ya kuwa na kipaji cha kuandika na kurap, COYO pia ana kipaji cha kuimba kama alivyofanya kwenye chorus ya wimbo huu.
Tizama video,sikiliza audio na kudowload
Post a Comment