0
Mashabiki wa kundi la Destiny’s Child wameanza kupata mshtuko baada ya kuona dalili zinazoonyesha kuonekana kurudi tena kwa kundi hilo. Hii ni ndoto ya muda mrefu kwa mashabiki wa kundi hilo.
Mshtuko mkubwa ulianza kuibuka wiki iliyopita baada ya kuonekana kufunguliwa kwa akaunti mpya ya mtandao wa Instagram inayotumia jina la kundi hilo ambayo mpaka sasa imefanikiwa kupata follower’s 32.2k na kuwa verified kwa muda mfupi zaidi.


Huu ni muonekano wa akaunti hiyo inayodaiwa ni ya Destiny Child

Kundi hilo linaloundwa na mastaa watatu akiwemo Beyonce, Kelly Rowland na Michelle Williams ambao waliachana mwaka 2006 na kila mtu kufanya kazi peke yake.

Post a Comment

 
Top