0
Muimbaji na mwalimu wa dance anayeishi nchini Ujerumani, Emanuel Austin, ameanzisha label yake – EMA Entertaiment.
Ameiambia Teamkazi  kuwa label hiyo tayari imechukua wasanii kutoka Ujerumani, Tanzania na Kenya. Austin amedai kuwa sababu ya kuanzisha label hiyo ni kutokana na kuona kuwa kuna vijana wenye vipaji lakini wamekosa watu wa kuwashika mkono.

Pia amedai kuwa wengi wamekuwa wakimtumia ujumbe wakitaka awasaidie.

Kwa upande wake Rajson Melody ambaye amekuwa miongoni mwa wasanii wa kwanza kuchukuliwa kwenye label hiyo, amesema ni kitu ambacho kinaweza kubadilisha maisha yake.

Austin amesema kuwa video ya wimbo ‘Mapenzi Digitali’ aliyomshirikisha Rajson Melody itatoka Ijumaa hii.

Post a Comment

 
Top