Muimbaji wa Uganda, Juliana Kanyomozi amefunguka kwa urefu kuhusiana
na masuala mbalimbali kwenye mahojiano aliyofanyiwa na mtandao wa SatisfashionUG.
Miongoni mwa mambo aliyohojiwa ni pamoja na kuvuja kwa picha za utupu za muimbaji mwenzie wa Uganda, Desire Luzinda. “Kwanza kabisa katika kesi nyingi kamwe huwa sio kosa la mwanamke,” anasema Juliana.
“Kama wewe ni mtu mzima na umempenda mtu unajua kuwa hakuna kikomo cha kipi kitatokea kwenye chumba binafsi cha watu wazima wawili. Kama hautaenda mbali zaidi kumfurahisha mwanaume wako, atakuacha na kisha utahukumiwa kwa hilo,” aliongeza.
“Pindi mwanaume anapovunja uaminifu na kuamua kushare vitu hivyo siri kwa dunia nzima na kutumia vyote dhidi ya mwanamke – ndio maana bado tuna safari ndefu kama wanawake kukemea tabia hiyo.”

Juliana alitolea pia mfano wa udukuzi uliofanyika nchini Marekani na kudai kuwa pamoja na picha za wasanii mbalimbali kuvuja hakuna chombo cha habari cha kuaminika kilichozianika.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.