“Nawashangaa sana hao wanawake si huyo Wema (Sepetu) wala hao wenziye, maana Diamond alisema kampa mimba Penny (Penniel Mungilwa) zikatoka huku mwenyewe akikanusha hajawahi kushika mimba kwa kumchafua tu mwanangu aonekane siyo mwanaume rijali,” alisema mzazi huyo.
Alisema kuwa kikubwa anachokiamini wote hawakuwa na upendo wa kweli kwa mwanaye, walitaka kuzitumia tu fedha zake na kumuacha solemba lakini sasa Zari ndiye mwenye penzi la dhati kwa mwanaye.
“Kiukweli Zari kanifurahisha. Ndiye mkwe wangu wa kweli na halali kabisa.
“Nampongeza sana Zari kwa kushika ujauzito wa mwanangu. Sasa Diamond atatembea kifua mbele kwa kujiamini,” alisema baba D.
Alisema kutokana na kile kilichokuwa kikiaminika kuwa hana maelewano mazuri na mkali huyo wa Bongo Fleva, kwa sasa wapo vizuri na hata akiwa na tatizo huwa anamwambia Diamond ambaye amekuwa akimpa msaada.
“Kwa sasa nina maelewano mazuri na Diamond, muda wowote nikiwa na tatizo huwa namjulisha ananisaidia, kitu ambacho kinamfanya amgharamie mama yake kuliko mimi ni kwa sababu aliishi naye kwa kipindi kirefu na kuhangaika naye tangu utotoni,” alisema.
Ukiacha Zari ambaye amekubali kubeba ujauzito wake, Diamond aliwahi kuwalalamikia baadhi ya wapenzi wake kuwa walikataa kumzalia mtoto akiwemo Wema, Penny na Jokate Mwegelo
Post a Comment