0
Kwa mara ya kwanza muigizaji na muongozaji mahiri wa filamu nchini ameingia kwenye skendo ya kugeza filamu ya nje na kutengeneza filamu yake iitwayo ‘Mzee wa Swagga’.
Issue hiyo ilianza kujulikana kwenye kipindi cha Take One cha Clouds TV ambapo kwa mujibu wa mtangazaji Zamaradi Mketema, shabiki mmoja wa show hiyo alimweleza kufanana kwa filamu hiyo na filamu ya kihindi ya mwaka 2011 iitwayo Ladies vs Ricky Bahl.



Filamu ya Mzee wa Swagga na Ladies VS Ricky Bahl inafanana kila kitu kuanzia story, aina ya wahusika na mengine.

Hata hivyo akizungumza na Bongo5 leo, JB amesema hawezi kuzungumza chochote kwa sasa kufuatia kubainika kwa mfanano huo wa filamu hizo mbili unaoshiriwa wazi kuwa filamu yake ni kopi ya filamu hiyo ya Kihindi.

“Sina cha kuzungumza hapa, nimesema siwezi kuzungumza chochote. Sijaki kuongea, mimi sasa hivi nachotaka sinema iuze tu,” alijibu JB kwa jazba.

Katika hatua nyingine, Bongo5 imezungumza na mmoja kati ya wahariri wa filamu hiyo, Sonnatah Abdalah kutoka kampuni ya kampuni ya Wood Vision Entrainment.

“Unajua sisi kama sisi kazi yetu ni kupokea stori kusoma na kuanza kushoot pamoja na kuedit,” amesema Sonnatah. JB alituletea kazi pale ameandika katunga yeye leo nimeanza kusikia kwamba ile filamu hajatunga yeye. Nimesikia watu wengi wanazungumzia hili suala. Mimi binafsi siwezi kuongelea kiundani hili suala kwa sababu mhusika ni JB na sisi alituchukua tufanye kazi tu,” ameongeza mwanadada huyo ambaye pia ni muigizaji.

Filamu ya ‘Ladies VS Ricky Bahl’ inamhusisha muigizaji Ranveer Singh anayewatapeli wasichana mbalimbali, Hivyo ndivyo JB anafanya pia kwenye Mzee wa Swagga.

Wahusika wakuu wa filamu ya Ladies VS Ricky Bahl, ni wanawake wanne pamoja na yeye mwenyewe Ranveer Singh na pia kwenye Mzee wa Swagga wahusika ni JB na wasichana wanne wakiwemo Wastara Juma, Welu Sengo, Cassie Kabwita wa Zambia na Tea.

Post a Comment

 
Top