Lady Jaydee ameshirikishwa na msanii mahiri wa Kenya wa muziki wa soul, Atemi Oyungu kwenye wimbo uitwao Moyo.
Kupitia Instagram, Jaydee amesema kuwa hajaandika chochote kwenye wimbo huo.
“Atemi ni msanii mwenzangu toka Kenya. Ana wimbo wake amenishirikisha unaitwa MOYO, sijaandika hata neno moja kwenye huo wimbo, niliukuta umeshaandaliwa, nikapewa sehemu zangu za kuimba tu, nikatekeleza,” ameandika Jaydee kwenye Instagram.
“Ujumbe uliomo usihusishwe na maisha yangu binafsi. Ni wimbo mtamu kweli kweli, utawagusa wengi kwa njia moja au nyingine. Kaeni tayari kuupokea #Moyo,” ameongeza.
Atemi ni msanii mashuhuri nchini humo na amekuwa akitumika kama jaji au mwalimu kwenye mashindano mengi ikiwemo Tusker Project Fame.
Home
»
Bongo star
»
kenya star
»
STORY
» Lady Jaydee ashirikishwa na msanii mahiri wa soul wa Kenya, Atemi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment