0



 Muimbaji anayefanya vizuri kwenye muziki, Barakah Da Prince amesema yeye na menejimenti yake Tetemesha amejipanga vizuri kuhakikisha

anaendelea kufanya vizuri. 

Akizungumza hivi karibuni katika show ya miaka 10 ya THT iliyofanyikia Escape 1, Barakah alisema yupo makini na atajitahidi kufanya kile kinachohitajika kwenye muziki wa sasa ili aendelee kufanya vyema zaidi. “Mimi najiitaga ni gari lenye mwendo wa pole lakini ni gari ambalo liko imara na linajielewa,” alisema. “Unajua kwanini nasema hivyo! kwa sababu nimejipanga vizuri ku-maintain game yangu.

 Ukiangalia tangu nitoe ‘Jichunge’ nilikuja nikatoa ‘Sio Fine’ nikapanda nimekuja na ‘Siachani nawe’ imepokelewa vizuri na imenipa nafasi nzuri zaidi tofauti na hapo nilivyokuwa nyuma. Kwahiyo mimi kabla sijatoa kazi, najaribu kuangalia kazi ambayo itaendelea ku-maintan game la muziki wangu nisishuke, nijaribu kuongeza fans wangu. 

Kwahiyo ni kitu ambacho nimejipanga sana mimi na menejimenti yangu, kwasababu tuna malengo makubwa na tunataka kufika mbali zaidi ya hapa na kuleta ushindani katika muziki wa Bongo Flava,” aliongeza. “Hii hali inanifanya niwaze kazi nzuri kwa sababu inafika hatua mpaka mimi nalinganishwa na akina Alikiba, akina Diamond ambao sasa hivi ni wasanii wa kimataifa. Kwahiyo ni kitu ambacho kinanifanya nifikirie kazi nzuri kila siku, nifanye kitu ambacho kitawateka watanzania na kufanya watanzania waniamini mimi ili kuongeza mashabiki wa muziki wangu.” “Pia hii hali inanifanya nisilale kwa sababu kinachofanywa nini nipendwe na mashabiki na nitabiriwe makubwa ni kazi nzuri. 

Kwahiyo inanifanya kila siku niwaze kazi nzuri na kubwa ambayo itafanya muziki wangu kwenda mbele na niongeze mashabiki East Africa, ikiwezekana Afrika na dunia nzima. Kwahiyo naishukuru Tetemesha media mbalimbali ambazo zinaniunga mkono kila siku pamoja na mashabiki wangu wa damu ambao kila siku wamekuwa wakiniumiza kichwa kuwapa kazi nzuri.”

Post a Comment

 
Top