“Happy” ni ngoma moja ambayo inaweza ikawa ni iliyofanya vizuri zaidi katika miaka 10 iliyopita, ngoma iliyobadilisha maisha ya Pharrell Williams miaka 10 baadae, baada ya kutokuwepo katika mainstream ya muziki kwa muda, ngoma hiyo ilikimbiza sana na kushika charts mbalimbali za vituo vya redio mbalimbali duniani audio pamoja na video yake, pia ngoma hiyo imempatia Pharrell tuzo kibao kubwa duniani ikiwemo tuzo ya grammy na mafanikio mengine makubwa katika kiwanda cha muziki.
Pamoja na hayo yote mtu mzima Pharrell ameona haijatosha inabidi kama ngoma hiyo iendelee kumuingizia mkwanja zaidi, amesaini deal ya kuchapisha kitabu na Putnam Books kwa ajili ya vitabu vya watoto, kitabu hicho cha kwanza kitakuwa kimetoka kutokana na wimbo huo wa “Happy” ambao umeshinda tuzo ya grammy.
Vitabu vinne vya mwanzo vya vitabu hivyo vya muendelezo (series), vitakavyoitwa “Happy” vitatoka Septemba 22, kitatumia picha za watoto kutoka sehemu mbalimbali duniani, kikimaanisha na kuwa na maana ya kuwa na furaha. Kutakuwepo na copies 250,000 vitakavyochapishwa na kusambazwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment