0
Baba mdogo, mama mdogo, kaka, mjomba na watoto wa kaka yake na rapper Stereo wamepoteza maisha kwenye ajali ya moto iliyotokea usiku wa kuamka leo kwenye maeneo ya Ukonga Banana jijini Dar es Salaam.


Nyumba iliyoteketea na kusababisha vifo vya baba mdogo, mama mdogo,kaka,mjomba na watoto wa kaka yake na rapper Stereo


Taarifa za ajali hiyo zimethibitishwa na watu wake wa karibu akiwemo Nikki Mbishi na Songa.

“Nimefiwa na baba mdogo (last born wa marehemu baba yangu),mama mdogo,kaka,uncle na watoto wa kaka yangu.Wameungua na moto usiku wa kuamkia leo,” Nikki Mbishi amenukuu ujumbe aliotumiwa na Stereo.

Bado haijafahamika chanzo cha moto huo na jitihada za kumtafuta Stereo zimegonga mwamba kutokana na simu yake kutopokelewa.

Tunampa pole Stereo kwa msiba huo mkubwa.

Post a Comment

 
Top