Mavoko ameelezea sababu za kukataa kutengeneza skendo ili kukuza biashara yake ya muziki.
“Mi nafikiri hatuwezi tukawa sawa, na kitu hichi mi nimekigundua kwa muda mrefu, watu wengi wananifata tufanye hichi tufanye hichi mi naweza nikafanya skendo na wewe siwezi kuwataja,” Mavoko aliiambia Amplifaya ya Clouds Fm. “Lakini mi nachoona hatuwezi tukawa sawa tutakuwa wote tumekuwa kwenye mlolongo ule ule, kuwa na skendo kwenye muziki wako kufanya biashara yako iwe nzuri ni style yako wewe kuwateka watu , sometimes inakuwa mbaya au nzuri pia. Lakini kwangu nikaona nikifanya hivi na yule anafanya na huyu nawe unafanya tunakuwa tunafanana, lazima niwe na lifestyle tofauti, naweza nikawa niko cool tu sitaki skendo staki nini napiga mangoma tu yanahit mi nimechagua style yangu iwe hivyo.”
“Kwetu pia ni mtuwa dini yaani ni mtu wa kanisani san asana sana, kuna vitu mama yangu pia havitaki aliniambia pia kwenye muziki nakuruhusu lakini kuna vitu moja mbili tatu staki…kwahiyo naogopa, wengine wananiambia biashara yako ndo itakuwa lakini naona No, bila nyimbo huwezi mimi kunijua…na sio kwamba anyefanya skendo anakosea yeye ndio style yake,” alimaliza Mavoko.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.