Mtangazaji wa Clouds FM, Millard Ayo na mshindi wa vipengele viwili kwenye Tuzo za Watu mwaka jana ni mtu wa mambo ya kimya kimya ndio maana picha ya studio aliyokuwa akiijenga nyumbaji kwake kwa mwaka mzima zimewashtua wengi.
Mtangazaji huyo wa kipindi cha Amplifaya anakuwa mtangazaji wa kwanza Afrika Mashariki kama si Afrika nzima kuwa na studio ya kisasa ya redio ndani mwake.
Hajasema kwanini ameamua kufanya hivyo lakini amedai hiyo ilikuwa ni ndoto yake ya miaka mingi.
“Siku zote ni furaha pale ndoto inapokua kweli, nilitamani sana siku moja kumiliki studio yangu ya radio kutokana na jasho langu na leo namshukuru Mungu nimefanikiwa kumaliza ujenzi wa studio yangu baada ya kudunduliza kidogokidogo kwa zaidi ya mwaka mmoja ndio maana hata wewe hutakiwi kukata tamaa kwa chochote hata kama kinachelewa mtu wangu, nilianza kuidizaini hii na baadaye watu wangu @francis_ayo na @abdul8819 wa @pixelbasetz wakanisaidia sana yani, nina mengine yanakuja ila kwa leo nimekupa hii tu mtu wangu! hapa panaitwa #TZA,” ameandika kwenye Instagram.
“Thanks kwa Maboss wangu Joe Kusaga, Ruge na @sebamaganga wamenipa nguvu na nafasi kubwa sana kwenye maisha yangu! birthday yangu ilikua Jan26 na nimejipa hii studio kama zawadi kubwa kwenye maisha yangu baada ya kuihangaikia usiku na mchana bila kukata tamaa.”
Hizi ni baadhi tu ya comments za followers wake kwenye Instagram:
1. Role model wa vijana weng TZ….plz usituangushe kwa hil for sure unastahik pongez sna kwa hil daaaah…safi sna @millardayo
2. Big up Millard upo clouds hata miaka miwili haijafika ushafanya mambo makubwa hivyo kuna wenzio wako karibia miaka kumi sasa hawana hata MIC
3. Kiukweli Millard huwa unanipa nguvu ya kusonga mbele na kuamini kuwa kila kitu kinawezekekana.am student nasomea masscommunication napata shida sana na kukata tama pale ambapo nanyimwa field nakudharaulika juu bt.name amini one day ntafika mbali zaidi na hawa wanaonidharau wataniheshimu nikutakie kila la kheri na hongera sana kaka angu kwa hatua hiyo.all the best@millardayo
4. U have totally inspired me to save more fo wat i want to accomplish before july
5. OMG I didn’t see this, @samchom thanks for the tag. Congrats Mill wange! I’m so proud of u! Hard work pays always! Hongeraa sana Mtu wangu wa nguvu @millardayo @mrs_mario30
Tunampongeza Millard kwa hatua hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment