0
Ajali mbaya imetokea Jumatano hii maeneo ya Mafinga mkoani Iringa katika kijiji cha Changarawe baada ya lori la mizigo lililokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Mbeya lililokuwa likikwepa shimo kubwa lililopo katikati ya barabara, kugongana na gari la abiria la kampuni ya Majinja lililokuwa likitoka Mbeya kwenda Dar es Salaam, kwa mujibu wa maelezo ya trafiki aliyekuwepo kwenye eneo la ajali.

Abiria wengi wamekandamizwa na kontena

Kontena la lori hilo limeilalia basi na watu wengine wamelaliwa huku wengine wakiporomokea kwenye korongo.



Kwa mujibu wa mtandao wa Jamii Forums, mpaka sasa hakuna majeruhi ni maiti tu wala hakuna mtu mtu anayedhaniwa kupona.

“Kuna watoto wawili hapa, makadirio ya miaka ni mitatu na saba, lakini hawa inasemekana kwamba walirushwa korongoni kutokana na huo mgongano,” imesema taarifa kwenye mtandao huo.



Uokoaji wa maiti na majeruhi walionasa kwenye ajali katika eneo la tukio unazorota kutokana na ukosefu wa gesi ya kukata basi kukosekana Mafinga. Juhudi zinafanyika ili kuweza kuokoa majeruhi pamoja na maiti.

Barabara ya kutoka Mbeya kabla ya kufika Mafinga imefungwa na zoezi la uokoaji linaendelea.

Tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza kutokana na picha hizi

Post a Comment

 
Top