0
Alhaji Sidiku Buari, baba wa kumlea wa muigizaji mrembo wa Ghana, Nadia Buari amechukizwa na tetesi kwenye vyombo vya habari nchini humo vinavyosambaza habari za uongo kuwa rais wa nchi hiyo, John Mahama ndiye baba wa watoto mapacha wa muigizaji huyo.
Buari ameelezwa kusikitishwa na ripoti kuwa Nadia alihojiwa na kudai kuwa rais huyo ndiye baba wa watoto wake mapacha waliozaliwa mwezi uliopita.

Kuzaliwa kwa watoto hao ambao wote ni wasichana kulizua mjadala mkubwa kwenye vyombo vya habari vilivyotaka kumjua baba wa watoto hao.

Kulikuwa na ripoti kuwa muigizaji Jim Iyke aliyewahi kuwa mpenzi wa Nadia kuwa si baba wa watoto hao na hivyo baadhi ya ripoti zikadai kuwa rais wa nchi anaweza kuwa baba wa watoto hao.

Post a Comment

 
Top