0
Juma Nature anaamini kuwa akiamua kugombe ubunge wa Temeke ataupata kirahisi.
Nature ameiambia XXL ya Clouds FM kuwa alishafuatwa na baadhi ya viongozi wamkita agombee nafasi hiyo.

“Walishanifuata watu, lakini kwa mwaka huu nimeona kwanza nikaushe,” amesema Nature. “Mimi mbona ubunge wa Temeke nakula, tena vizuri kabisa, bila hata matatizo. Kwa vyama mbalimbali siwezi kuvitaja, nimeacha kwanza akina Professor wachukue kwanza, lakini baadaye miaka mingapi usije ukashangaa nipo mjengoni, nimevaa suti kali,” aliongeza msanii huyo.

Nature alisema akiwa mbunge wa Temeke ataanza kushungulia miundo mbinu ya barabara pamoja na ujenzi holela ambao umekuwa ukisababisha mafuriko mara kwa mara.

Post a Comment

 
Top