0
Hatimaye probation ya Chris Brown (25) kwenye kesi yake ya kumpiga aliyekuwa girlfriend wake wa wakati huo Rihanna imemalizika, na sasa amemalizana kabisa na kesi hiyo ikiwa ni miaka sita na mwezi mmoja toka atende kosa hilo mwaka 2009.
Breezy ameshare habari hiyo kupitia Twitter kwa kuandika “IM OFF PROBATION!!!!!!!! Thank the Lord!!!!!!”



Staa huyo wa hit single ya ‘Loyal’ alikuwa akikabiliwa na kesi ya kumshambulia Rihanna Feb. 8, 2009 ambapo baada ya kukutwa na hatia alikubali kufanya kazi za jamii ili kukwepa kwenda jela.

Post a Comment

 
Top