0
Godzilla anafurahia zaidi kujisimamia mwenyewe na anaamini kuna faida zaidi kuliko kuwa na menejimenti.
Rapper huyo ambaye leo anaachia wimbo wake mpya ‘Nobody’ ameiambia Bongo5 kuwa hasara ya msanii anayesimamiwa ni kuwa uongozi huo ukimwacha hujikuta katika wakati mgumu na wengi hushindwa kuendelea.

“Inabidi kwenda mwenyewe ili msanii anajua kabisa akiwa anamhitaji mtu anamfuata mwenyewe,” amesema. “Hapo unakuwa unajua pakuanzia na pakuishia.”

“Menejimenti ikikuacha unabaki hujui wapi pakuanzia and you career is finished. Na watu wengi walioanguka ni wale ambao walikuwa wakitegemea kufanyiwa kila kitu, inabidi kujitegemea mwenyewe.”

Msanii huyo amesema kwa kipindi chote amekuwa akisimamia kila kazi inayohusiana na muziki wake japo amemtaja Marco Chali kama mtu ambaye amekuwa naye karibu hasa katika masuala ya kurekodi.

Post a Comment

 
Top