Rapper wa TMK, Inspekta Haroun anatarajia kwenda nchini Japan kwenda kutengeneza ngoma na video mpya.
Inspekta ameiambia Bongo5 kuwa hivi karibuni alituma picha za video aliyoifanyia nchini kwenda kuhaririwa Japan lakini zimeonekana kuwa na ubora mdogo na hivyo kulazimika kwenda mwenyewe.
“Ile kampuni ya Japan wamekataa kutumia picha tulizowatumia, wamesema hazina ubora sijui tumetuma kwa njia ya mtandao. Lakini wananipa ofa ya kwenda kufanya video mbili na audio huko huko Japan, wao wameniambia niende mwezi wa sita, kwahiyo najiandaa mwezi wa sita niende. Itakuwa kazi mpya kabisa ambazo watu hawajaziona,” alisema rapper huyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment