0

Kuelekea mpambano wa watani wa jadi katika
mchezo wa mpira wa miguu hapa nchini, mchezo
kati ya Simba na Yanga ambao utafanyika hapo
kesho kwenye uwanja wa taifa jiji Dar, Staa wa
Bongo Movies, Jacob Stephen ‘JB’ ambae ni
mshabiki “kindakindaki” wa timu ya Simba
amemtaka Staa mwenzake Vicent Kigosi ‘Ray’
ambae ni shabiki wa Yanga, aweke dau shilingi
milioni moja kama alivyofanya mchezo uliopita na
yeye JB ataweka milioni mbili, kama Yanga
ikishinda Ray atachukua mzigo na kama Simba
ikishinda JB atachukua mzigo huo.
“Weka milion, mimi naweka mbili sheria zinasema
mwenye uhakika wa ushindi ana point chache.si
haki tukiweka sawa..si unakumbuka mara ya
mwisho tulipokutana.jaribu tena urudishe hela
yako...”-JB aliandika na kumtag Ray mara baada
ya kuweka picha hiyo wakiwa pamoja.

Post a Comment

 
Top