“Unajua siasa ni ngumu mimi bado nipo kwenye mjadala wa kugombea na hii ni baada ya kuona watu wanataka kuongozwa, lakini bado nafikiria,” amesema. “Nikiwa tayari nitagombea kupitia CCM. Kitu ambacho kinaniogopesha kiukweli ukiangaliwa watu waliopita ni vijana tu wanakufa mapema kutokana na mambo ya siasa. Siasa inahitaji moyo sana mimi ni muoga sana, naogopa kufa watu wanauwana! Mtu unatamani lakini ndo hivyo,” ameongeza.
“Mimi napigiwa simu nyumbani Igunga, watu wengi sana kila mmoja ananiambia ‘tunakuhitaji ugombe yaani baada ya Rostam wananihitaji mimi! Mimi bado nipo njia panda mpaka sasa hivi lakini muda ukifika kila kitu mtasikia.”
Post a Comment