Bobbi Kristina. Bobbi Kristina ambaye ni mtoto wa nguli wa muziki Bobby Brown na marehemu Whitney Houston, amezinduka baada ya kupoteza fahamu kwa zaidi ya miezi miwili kutokana na kilichoelezwa kuwa ni matumizi ya dawa za kulevya.
Binti huyo alikuwa mahututi kwa zaidi ya siku 75 na alikuwa akipatiwa matibabu baada ya kukutwa ndani ya jakuzi nyumbani kwake januari 31, mwaka huu akiwa hajitambui.
Kupitia ukurasa wa Facebook, Brown aliandika: “Kweli Mungu ni mkubwa, mpenzi wangu, binti yangu amefumbua macho na kunitazama. Ndiyo, hatumii mashine ya kupumulia tena, anapumua mwenyewe ingawa bado anapatiwa matibabu.
(Chanzo: MTV)
Post a Comment