0
Muimbaji Justin Bieber amemfanya rapper Big Sean kupata wivu na wasiwasi kuwa huenda akaibiwa tunda lake, baada ya muimbaji huyo wa Canada kumkumbatia girlfriend wa rapper huyo Ariana Grande jukwaani.
Ariana alikua akitumbuiza huko Los Angeles, Marekani Jumatano wiki hii na Bieber alipanda jukwaani kama ‘surprise’ na kutumbuiza naye.



Wakiwa wanaimba pamoja Bieber alimkumbatia na kumshika kimahaba Ariana kama couple, kiasi cha kumfanya Big Sean apatwe na wivu na kushindwa kuvumilia. Inasemekana kuwa Sean alitumia Twitter kumchimba mkwara Bieber kwa kuandika, “huyu mtoto anatakiwa ajifunze kutomshika hivyo msichana wangu”, tweet ambayo inaaminika baadaye ilifutwa.



Hata hivyo vyanzo vingine viliuambia mtandao wa TMZ kuwa tweet hiyo ilikuwa feki.



Post a Comment

 
Top