0
Kampuni ya Universal Pictures International imeshaingiza dola bilioni 1 zilizotokana na mauzo ya tiketi za kutazama kazi zake zilizotoka mwaka 2015.
Kwa mujibu wa mtandao wa Forbes, kiasi hicho kimetokana zaidi na mauzo ya tiketi ya kuitazama filamu ya Furious 7 iliyoingiza dola milioni 316 nje ya Marekani katika wiki ya kwanza.

Furious 7 inakuwa filamu ya nne kuwahi kuingiza fedha nyingi zake duniani katika wiki yake ya kwanza na kuna uwezekano mkubwa kuwa Fast & Furious 7 ikaingiza hadi dola bilioni 1 hivi karibuni.

Hiyo ni pamoja na ukweli kwamba filamu hiyo tayari imeshapakuliwa kiuharamu mtandaoni kwa zaidi ya mara milioni 2.5 kupitia sites za torrent.

Filamu nyingine ya Fifty Shades of Grey imeisaidia Universal kuiingiza dola milioni 401.2 duniani tangu izinduliwe kwenye Valentine’s Day wakati filamu ya The Theory of Everything ikiwa imeingiza dola milioni 85.

Post a Comment

 
Top