0
Staa wa Nigeria, David ‘Davido’ Adeleke ambaye anatokea kwenye familia bora na aliyepata mafanikio makubwa kupitia muziki, aliwahi kuacha shule mwaka 2011 ili afanye muziki. Lakini baada ya kupata ushauri na kugundua umuhimu wa elimu alikubali kurudi shule na hatimaye sasa anakaribia kuhitimu.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Davido ameshare furaha yake ya kumaliza mitihani na sasa anakaribia kuhitimu shahada yake ya kwanza June 7, 2015.

Davido ameandika kuwa mwaka mmoja baada ya kuacha shule mwaka 2011 huko Marekani, baba yake alimtaka amalizie elimu yake hata kama tayari amefanikiwa kimaisha, kitu ambacho Davido anasema yeye haikumuingia akilini kwasababu alikuwa na pesa, magari, majumba na umaarufu. Lakini baada ya kupata ushauri kutoka kwa ndugu na marafiki alifanikiwa kurudi na sasa anafuraha kuikamilisha safari ambayo anadai ilikuwa ndefu na ngumu.

Kupitia Instagram ameandika:

“LAST PAPER DONE!!!! FINALLY ABOUT TO BE A GRADUATE !!! BEEN A LONG AND HARD JOURNEY I WONT LIE! I REMEMBER DROPPING OUT OF SCHOOL IN AMERICA 2011 FOR MUSIC. AFTER A YEAR MY DAD DEMANDED THAT I FINISHED MY EDUCATION EVEN THOUGH SUCCESS HAD COME MY WAY ! IT DIDNT MAKE SENSE GOING BACK TO ME , I HAD IT ALL IN MY EYES , HOMES, CARS , MONEY NAME IT !! BUT AFTER ENCOURAGEMENT FROM MY PEERS AND FAMILY MEMBERS IM FINALLY DONE AND IM HAPPY TO SAY THIS DEGREE IS MY MOST CHERISHED ASSET!! WE DID IT!! #BADDESTNIGGAWITHABSC EAGLE GRADUATING CLASS BABCOCK UNIVERSITY!!! GRADUATION DAY 7th OF JUNE!!!”

Post a Comment

 
Top