0
Inavyoonekana kuna mashabiki wa rapper Mabeste ambao hawakufurahishwa na uamuzi alioutoa miezi kadhaa iliyopita wa kuweka muziki pembeni kwa muda ili apate muda wa kutosha kumsaidia mke wake ambaye ni mgonjwa.
Mabeste ameandika ujumbe mrefu kupitia akaunti yake ya Facebook akisema kwamba anashangaa kuona baadhi ya mashabiki wake wanaosema kuwa toka aoe amepoteza mwelekeo kwenye muziki, hivyo ndoa ni kama imempotezea baadhi ya mashabiki kwasababu haupi tena muziki kipaumbele.

Hiki ndicho alichoandika Mabeste:

“Mziki ni kazi yangu na si sehem ya ufuska au kupata madem…..kipaji changu ndo kinaniletea fans na biashara yangu kukua! Sidhani kama isingekua kipaji changu mngemjua MABESTE!! Ama mi nili hit kwa vile nilikua na madem??? So wale ambao mnasema mtu akioa anapoteza fans, Me nakataa kabisa kama kipaji kipo … kipo tu!!! Hata usipoachia nyimbo kwa game miaka 20 ukija kuachia kipaji kitaonekana tu!!! Music its all abt kipaji & promotions si madem wala skendo!!

So me nashangaa sana mnaosema eti nimeloose kisa nampenda mke wangu!!! Jamani Siwezi ishi maisha fake au kuishi watakavyo watu!!! Kwani apart from my Music I have my personal life!!! So mlitaka nimuache mtoto wa watu ateseke peke yake anaumwa kisa fans jamani?? Kwani kazi duniani ni music peke yake???? wajameni mnamjua vizuri lisa??? Je mnajua what she is going through au anavumilia mangapi ktk maisha yetu!!??

Sasa kama fans wa kike mtaacha kupenda mziki wangu kisa nampenda mwanamke mwenzenu its fine with me….niko radhi kua na fans wachache lakini wa uhakika!! Pia nita washangaa kwa hilo coz mnatulalamikia artist sisi ni player’s! Pia wanaume sisi sio waaminifu! Sasa hata sisi ambao wakweli pia tunasemwa!!!

Yes nimeachia mziki wangu kwa mda ili wife wangu akae sawa na kumuomba MUNGU ampe afya!! Pia namheshim MUNGU saana Coz nilimuomba miaka mingi hapo nyuma anipe msichana nitakaye fanya nae maisha nisije angamia kwa hii industry maana Vishawishi ni vingi mapenz ya uongo mengi..MUNGU alisikia kilio changu akanipatia a woman of my dreams! ! Na Jambo zuri pia ni lazima lipite ktk mitihani so huu mtihani MUNGU alionipa ni lazima niupite coz nilichomuomba amenipatia how do I value it lazima kupita kwa ups & downs!!!

Stop talking shits na hit kwa mziki wangu, niko na kipaji na si madem wala skendo!!!Enyi wajinga wacheni ujinga mkaishi coz siri ya ndoa sio tendo la ndoa..Nawapenda saana peace… Easter njema”

Post a Comment

 
Top