0
Floyd Mayweather amesema pambano dhidi yake na Manny Pacquiao litakutanisha ‘mahall-of-famer’ watarajiwa ambapo litaweka historia ya kuwa pambano litakaloingiza fedha nyingi katika historia ya masumbwi.
Floyd Mayweather akifanya mazoezi pamoja na mjomba wake Roger kwenye gym Las Vegas

Pambano hilo, litapigwa May 2 kwenye ulingo uliopo MGM Hotel jijini Las Vegas.



Akiongea na waandishi wa habari Jumanne hii jijini Las Vegas, Mayweather alisema hahofii kuharibu rekodi yake ya kutopigwa katika mapambano 47-0.


Mayweather akiongea na waandishi wa habari

“Yeye ni hall-of-famer wa baadaye. Mimi ni hall-of-famer na tunakutana katika kilele cha career zetu,” alisema Mayweather.


Mayweather akipasha mbele ya waandishi wa habari aliowaalika kambini kwake


“Naamini litakuwa pambano la kuvutia. Style zetu ni tofauti kabisa. Napigana kwa umakini. Kila mwendo umepigiwa mahesabu. Kila mwendo umefikiriwa.”


Mazoezi si marahisi



Kwenye pambano hilo Mayweather atalipwa takriban dola milioni 120 na Pacquiao atapokeza dola milioni 100.



Bondia huyo alialika waandishi wa habari na mastaa wengine kushuhudia mazoezi yake.


Lil Kim ni miongoni mwa mastaa waliohudhuria mazoezi ya bondia huyo wiki hii









Post a Comment

 
Top