0
Cassim Mganga ambaye kwa sasa anafanya vyema na wimbo wake ‘Subira’ aliomshirikisha Christian Bella, amesema video ya wimbo huo itafanyika Tanga.
Akiongea na E-News ya EATV, Cassim alidai kuwa awali alipanga kwenda kuifanyia nje ya nchi lakini amebadilisha mawazo na kuamua kwenda kule mapenzi yalikozaliwa!

“Video tunafanya mwezi huu na Mungu akipenda nitaiachia mwezi huu mwishoni na itafanyika Tanga,” alisema.

“Mwanzo tulikuwa na presha ya kwenda kuifanya nje ya nchi lakini baadaye wadau na marafiki walitoa mawazo yao kuwa tuifanye tu hapa hapa maana ni wimbo ambao una mahadhi ya kinyumbani zaidi pia una midundo ya asili ya pwani. Ni wimbo ambao unahitaji uoneshe maudhui ndio tukaona ifanyike Tanga,” aliongeza.

Post a Comment

 
Top