0
Mwanamuzi wa bendi ya Malaika, Christian Bella anaamini kuwa Belle 9 ni msanii mwenyezi uwezo mkubwa ila tatizo hana tu nyota ya kung’aa.
Hivi karibuni Bella alikuwa kwenye kipindi cha ‘Mboni Show’ ambako alisema Belle amekosa nyota ya kung’aa ingawa ana uwezo mkubwa wa kuimba kwa kutumia sauti yake.

“Sielewi kwanini rafiki yangu Belle 9 ana nyimbo kali na sauti yake inakubalika sana, lakini sijui tatizo ni nyota au vipi, napenda sana kazi zake, ni staa kwangu,” alisema Bella.

Bella pia alisema wasanii wengine wanaomvutia ni Diamond na Alikiba.

“Nisiwe mnafiki, Diamond hana sauti nzuri kama Alikiba katika kuimba na Alikiba nimeshawahi kufanya naye kazi kwa kuimba ‘live’ sauti yake ni ile ile, ni msanii mwenye uwezo mkubwa wa kuimba ‘live’ lakini Diamond ni mjanja wa kuichezea sauti yake na anafanikiwa kutangaza nchi kimataifa, lazima apongezwe kwa hili.”

Source: Mtanzania

Post a Comment

 
Top