0
Diamond Platnumz, Ommy Dimpoz na Alikiba si wasanii pekee wa Tanzania wenye mashabiki lukuki Kenya! Msanii mwingine mwenye fan base ya hatari nchini humo ni Rich Mavoko.
Rich Mavoko akiwa na mchekeshaji wa Kenya, Jalang’o

Kuna kitu cha pekee alichonacho staa huyu ambacho kimemsaidia kupata mashabiki wengi nchini humo. Ni nyimbo zake tamu zenye uandishi ambao wakenya huupenda! Ni hivi karibuni tu, Mavoko aliligundua hilo, kwamba jina lake linatajwa mno na nyimbo zake zinafahamika na kuamua kutumia nafasi hiyo.


Rich Mavoko akitumbuiza Kenya hivi karibuni


Ni Hussein Machozi ambaye kwa miaka mingi amekuwa akiishi Kenya, aliyempa siri hiyo. Machozi alimwambia Mavoko kuwa kuna watu wengi wanaendelea kufaidika na muziki wake bila yeye kujua chochote.

“Nimekuta mdundo.com kuna mtu anachukua hela zangu tangu miaka mitatu nyuma, tangu nyimbo ya Silali. Sio hela ndogo, ni dola kadhaa. Yule jamaa alienda kujitambulisha kwamba yeye ni meneja wangu,” Mavoko aliiambia Bongo5 hivi karibuni.

Kwa kulitambua hilo, ndio maana aliamua kusaini mkataba wa usimamizi na kampuni ya Kaka Empire kusimamia kazi zake nchini Kenya.
Ni uongozi wa kampuni hiyo iliyoanzishwa na rapper Rabbit ndio uliomtafuta Mavoko na kupendekeza deal hilo.

“Kwahiyo jamaa wakaniambia kwamba hakuna mtu anayeweza kufuatilia vitu vyako vya Kenya kwahiyo inabidi upate wakala au mtu anayeweza akasimamia kazi zangu za Kenya naye atakuwa anachukua asilimia lakini haki zako zote unazipata,” alisema staa huyo.

Tayari matunda ya mkataba huo yameanza kuonekana. Mavoko ameanza kutumia umaarufu alionao Kenya kujiongezea nguvu.



Hivi karibuni alikuwa miongoni mwa wasanii waliosindikiza uzinduzi wa album mpya ya CEO wa Kaka Empire, Rabbit. Wasanii wengine waliopanda jukwaani ni pamoja na Bahati, Wyre the ‘Love Child’, Collo na wengine.

Mavoko pia alialikwa kwenye show ya comedy ya mchekeshaji maarufu wa Kenya, Jalang’o iitwayo ‘JALANG’O WITH THE MONEY’.

Alipost picha kwenye Instagram akiwa na mchekeshaji huyo na kuandika:

Wengi wanaoheshimika leo walishawahi dharaulika uko nyuma jua umuhimu wa nafasi anazokupa Mungu kuna aliyezichezea nawe umepewa kwa sababu fanya mpaka asiyetaka ufanye akwambie we noma na usiridhike na maneno yao wakisema hapo ndo mwisho wako wakati wao hawajuhi mwisho wao #wakatishaji_tamaa ni maadui wa maendeleo.”

Post a Comment

 
Top