0
Kanye West na paparazzi aliyemshambulia wamemaliza tofauti zao kwa kumuomba msamaha na kushikana mikono.
West alishtakiwa na Daniel Ramos baada ya mwaka 2013 kumshambulia wakati akiwa kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Los Angeles na kesi hiyo ilikuwa isikilizwe wiki ijayo.

Wakili wa Ramos, Gloria Allred aliandika maelezo jana Jumanne kuwa kesi hiyo imemalizika na kwamba Kanye alimuomba msamaha mteja wake.

Allred alituma picha ya West, akitabasamu wakati akishikana mkono na Ramos.

Post a Comment

 
Top