0
Cash Money Records inazidi kupukutika. Baada ya Busta Rhymes, sasa Bow Wow naye amewaaga bye bye!
Rapper huyo mwenye miaka 28 alitangaza kujiondoa kwenye label hiyo aliyosaini nayo miaka mitano iliyopita kupitia ukurasa wa Facebook.

Amesema kuwa hana tatizo na Cash Money wala Birdman ambaye alimshukuru kwa kumsainisha. Amedai kuwa akiwa Cash Money hakuwa na uhuru wa kuamka muda wa kutoa nyimbo zake japo zipo kibao alizoishia kuzisikiliza tu.

“I wanna dictate when my music comes out. I’m tired of going to the studio to make records and then I listen to them. ‘Cuz they get old… I just can’t be held up by nobody. It’s as simple as that,” alisema.

Baada ya kuondoka kwenye label hiyo, Bow Wow amesema atarudi kufanya kazi na Snoop Dogg na Jermaine Dupri waliogundua na kukikuza kipaji chake.

Post a Comment

 
Top