American Idol – show maarufu kwa kusaka vipaji vya waimbaji nchini Marekani inatarajiwa kusitishwa.
Show hiyo ambayo ni baba wa show zote za aina hiyo zikiwemo “The Voice” na “The X Factor” itasimama rasmi mwakani baada ya kumaliza msimu wake wa 15.
“Idol” ilianza mwaka 2002 na katika kilele chake iliwahi kuvutia watazamaji takriban milioni 30 kwa msimu.
Wasanii waliotoka kwenye show hiyo ni pamoja na Carrie Underwood, Kelly Clarkson, Jennifer Hudson, Jordin Sparks, Ruben Studdard, Fantasia Barrino ma Taylor Hicks.
Msimu wa mwisho utaanza January mwakani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment