0
Rapper mkongwe Joseph Haule aka Professor Jay amesema siasa haiwezi kumtenganisha na muziki, na pia amejipanga kuja na project mpya ya muziki iitwayo ‘The Icon’.

Professor akiwa kwenye shughuli za kisiasa Professor amesema kuwa, hata kama akipata nafasi ya ubunge atahakikisha mashabiki wake wanapata muziki kama kawaida.

“Nitaendelea kuwatumikia mashabiki wa muziki wangu kama kawaida, najua sasa hivi nadeni kubwa kwenye muziki, lakini hivi karibuni nitaachia kazi mpya kwa sababu hata huku nilikoingia nimeingia kutokana na muziki, kwahiyo hata nikiingia bungeni bado kazi nitaendelea kufanya, najua mashabiki wangu wanategemea muziki wetu kama chakula cha ubongo kwahiyo mimi bado nipo kwajili ya mashiki wangu,” alisema Professor.

Pia Professor Jay amejipanga kuachia project yake mpya ya muziki ‘The I Con’ ambayo itazungumzia maisha ya muziki wake ambayo itawashirikisha wasanii wengine.

“Hii project itamuonyesha Professor Jay alikotoka mpaka alipofikia, kwa sababu naamini Professor Jay ni role model wa wasanii wengi na vijana wengi wa Tanzania, pia nimekuwa mfano bora kwa wasanii wenzangu na vijana wengi wa Tanzinia, nimesabisha vijana wengi kuingia kwenye muziki kutokana na harakati zangu, hata vijana wengi ukiwauliza nani amekufanya ukaingia kwenye muziki utaambiwa ni Professor Jay, especial wanaofanya Hip Hop na vitu kama hivyo. Pia mafanikio yangu yamewafanya vijana wengi kuingia kwenye muziki hata wasanii wa kuimba, pia wazazi wengi nimejaribu kuwaaminisha kwamba muziki siyo uhuni na kuamua kuupenda, kwaiyo hizo harakati zangu zote kwa umoja wake utaziona kwenye The Icon, ndani ya project hiyo utakuta documentary yangu, albam na mambo mengi sana, kwahiyo hii yote inakuja ndani ya mwaka huu wadau na mashabiki wa muziki wangu wakae mkao wa kula,” alimalizia Professor Jay.

Post a Comment

 
Top