0
Mvumilivu hula mbivu! Licha ya kuandamwa na mashabiki kila kukicha, msanii wa bongo fleva Nuh Mziwanda ameanza kupata matunda ya uhusiano wake na Shilole kwenye muziki wake, sasa ameanza kula mashavu ya show za nje ya nchi ambazo hapo kabla alikuwa akienda Shilole peke yake.
Kwa mara ya kwanza Shilole na Nuh Mziwanda watasafiri pamoja kwenda Ubelgiji kwenye show watakayofanya May 9, 2015.


Lakini show hiyo itatanguliwa na show nyingine ya Shilole na Nuh jijini Durban, Afrika Kusini May 2, 2015.

Kupitia mahojiano mbalimbali Nuh Mziwanda aliwahi kukiri kuwa Shilole amekuwa msaada mkubwa katika muziki wake na maisha kwa ujumla.

Post a Comment

 
Top