0
Afrika ikae tayari kupokea collabo nyingine kutoka kwa Diamond Platnumz na Davido, japo haijafanywa lakini uongozi wa Diamond umesema kuna mpango huo.
Baada ya kuwepo kwa hisia miezi kadhaa iliyopita kwamba Diamond na Davido hawapatani tena, meneja wa msanii huyo Babu Tale amesema kuwa wasanii hao wataingia studio hivi karibuni ikiwa pia ni kama ishara ya kuwa hakuna beef yoyote kati yao.

Akizungumza na mtangazaji wa Citizen Radio ya Kenya, Willy M. Tuva, Tale amewahakikishia mashabiki wa Diamond kuwa hakuna matatizo yoyote kati yao, baada ya kuulizwa kama wana beef.

Alipoulizwa kama Diamond ana mpango wowote wa kufanya collabo nyingine na staa huyo wa Nigeria alijibu “Kuna kitu kitakuja cha Diamond na Davido…itafanyika soon tuseme Inshallah”.

Post a Comment

 
Top