0
Hit maker wa ‘Hakunaga’, Suma Lee amesema kuwa hatafanya tena muziki kwasababu ameachana kabisa na maisha hayo.
Image result for suma leeSuma ambaye alitengeneza pesa nyingi kupitia hit yake ya ‘Hakunaga’, amesema kuwa hana mpango wa kuzitoa nyimbo zake zilizoko studio ambazo hazijatoka.

“sifanyi tena muziki na nimeachana kabisa na maisha hayo, na nyimbo zote zilizobaki studio nimezisimamisha zisitoke baada ya kuzilipia, “ Alisema Suma.

“kuna wimbo mmoja nimefanya na Cp ambao ndio ulikuwa wa kurudisha kundi la Parklane, pia nimeuzuia, labda Cp auchukue yeye.Kilichobaki ni kuwaombea wazazi wetu waliotutangulia, wengine walikuwa hawataki tufanye kazi hizi, kwa kuwa hawapo na hakuna wakutukataza tena, bora tukae na kuwaombea.”

Post a Comment

 
Top