0
WAKATI staa wa Bongo Movie, Wema Sepetu akiweka wazi kuwa hawezi kupata ujauzito huku Judith Wambura ‘Jide’ naye akisumbuliwa na tatizo hilo, nyota wa muziki Rehema Chalamila, Ray C amefunguka na kusema kuwa hali ya kukosa mtoto ambayo ni sawa na ugumba, inamtesa, kwani katika umri wake wa miaka 33, hajabahatika kuwa naye,Risasi Jumamosi linakujuza.

Nyota wa muziki Rehema Chalamila, Ray C. Akizungumza na gazeti juzikati, Ray C alisema kuwa pamoja na hamu yake ya muda mrefu ya kupata mtoto, lakini ameshindwa ingawa anaamini siku yoyote Mungu atamuwezesha jambo hilo.“Hao kina Jide, Wema mi naona kama ni cha mtoto.  
Katika uhusiano wangu wa kimapenzi tangu nivunje ungo, nimewahi kushika mimba mara moja tu, wakati huo nikiwa na Mwisho Mwampamba, lakini bahati mbaya ilitoka, tokea hapo sijapata tena,” alisema staa huyo ambaye yupo katika mapambano ya kuacha matumizi ya madawa ya kulevya.
Alisema katika umri wake huo anatamani sana kuwa na mtoto, kwani wasichana aliozaliwa nao wakati mmoja hivi sasa wanao watoto wawili hadi watatu, kitu ambacho kinamuumiza.

Alipoulizwa kama matumizi ya dozi ya kuacha madawa ya kulevya inachangia tatizo lake hilo, alisema siyo kweli, kwani miongoni mwa ‘mateja’ wenzake anaokunywa nao dawa, wapo wajawazito na wengine wenye watoto.

Hata hivyo, alisema umri wake siyo mkubwa sana kukata tamaa ya kutozaa kwani wapo baadhi ya watu hupata ujauzito na kuzaa katika umri wa miaka 45 na kuendelea.“Sidhani kama umri ni sababu, nafikiri bado nina muda wa kuzaa na kumlea mwanangu nikijaaliwa kuwa naye, lakini pia huwa siishi kumshukuru Mungu kwa hivi nilivyo maana yawezekana kuna jambo ananiepusha nalo,” alisema.
“Kitu kingine kinachonifanya nisipate mtoto mapema ni pamoja na kutopata mwanaume aliyetulia ambaye ninaweza kuzaa naye, nadhani nikimpata mambo yanaweza kwenda vizuri.”Ray C anaingia katika orodha ya masupastaa ambao licha ya umri wao kuwa mkubwa, lakini bado hawajabahatika kupata watoto, baadhi yao wakiwa ni pamoja na Judith Wambura ‘Lady Jaydee’, Baby Madaha na Jacqueline Wolper.

Post a Comment

 
Top