0
Christian Bella amesema video ya wimbo wake mpya ‘Nashindwa’ ndio bora zaidi kuliko zingine za muziki wa dansi nchini na kwamba imemgharimu shilingi milioni 17.

Bella ameliambia gazeti la Mtanzania kuwa ubora huo unatokana na kuwekeza milioni 17 kwaajili ya video hiyo iliyofanyika nchini Afrika Kusini.

Alisema gharama hizo zinatokana na usafiri, maandalizi yote na kukamilika kwa video hiyo ambayo ipo katika kiwango cha kimataifa.

“Ukweli ni kwamba, tunatakiwa tubadilike tuwekeze kwenye video zetu si wa Bongo Flava tu nasi wa dansi tufanye hivyo, maana gharama kubwa ya video ya muziki wa dansi ni milioni 5,” alisema.

Post a Comment

 
Top