0
Muimbaji wa Kenya, Esther Akoth maarufu kama Akothee anafahamika kwa moyo wake wa kujitolea.

Akothee
Wiki hii muimbaji huyo ameahidi kulipitia tiketi ya ndege ya kwenda na kurudi India kwaajili ya mama yake na muimbaji maarufu wa Kenya, Size 8. Mama huyo aitwaye Esther Njeri anatakiwa kwenda nchini India haraka kwenda kubadilishiwa figo zake (kidney transplant).



Kutokana na gharama kubwa za matibabu, Size 8 na mume wake Dj Mo waliamua kuanzisha kampeni za kuchangisha fedha za matibabu iliyopewa jina ‘Simama na Mama Size 8’ ambayo Jumapili ndio ilikuwa kilele chake.

“Pole kwa ugonjwa wa mama yako, niwie radhi sikuweza kufika Jumapili kwa hafla ya uchangishaji fedha,” Akothee anasikika akisema kwenye sauti aliyorekodiwa na mtandao wa Mpasho.

“Ninachoweza kufanya ni kwa kulipia gharama ya tiketi ya ndege (kwenda na kurudi) kwa mama yako kwenda India. Namwombea apone haraka, Mungu awe nawe,” aliongeza.

Kwa mujibu wa Size 8, gharama za matibabu ya mama yake ni takriban shilingi milioni 36, kiasi ambacho hawezi kukimudu yeye mwenyewe.

Mastaa mbalimbali wa Kenya walijitokeza kwenye hafla hiyo wakiwemo Jaguar, Pierra Makena, Wambui of Elani, Wahu, Nameless na wengine.

Katika hatua nyingine Jumapili hii Akothee ataachia wimbo wake mpya kwaajili ya akina mama duniani uitwao ‘Sengerera Mama’.

Post a Comment

 
Top