Ili video ya msanii yeyote wa Tanzania iweze kuoneshwa kwenye vituo vikubwa vya TV vya kimataifa kama MTV Base, Trace au Channel O, sio lazima ifanyike Afrika Kusini au itengenezwe kwa gharama kubwa kama wengi wanavyodhani.
Kumekuwepo na dhana iliyojengeka miongoni mwa wasanii wa kibongo kuwa ili video zao zipokelewe na kupitishwa na vituo vya runinga vya kimataifa, ni lazima kuwatumia madirector wakubwa wa nje, na pia lazima ihusishe gharama kubwa, na wengine wakiamini kuwa msanii mwenye video iliyofanyika hapa nyumbani na director wa hapa hawezi kupata nafasi kwenye vituo hivyo.
Bongo5 imemtafuta Ambwene “AY” Yesaya, ambaye ametueleza kuwa gharama na sehemu ilipofanyika video sio vigezo vinavyotumiwa na vituo hivyo kupitisha video wanazopokea.
“Jinsi ambavyo vituo vikubwa vya Televisheni vya nje hupokea kazi ni kuwa haijalishi hiyo video imetengenezwa kwa milioni 50 au imetengenezwa milioni 1, ni jinsi tu ulivyopanga content yako the way ambavyo video yako imekaa vizuri, na kikubwa ni kuwa ufate masharti ya vitu ambavyo wanavihitaji. ”
AY amesema kuwa vituo hivyo vya kimataifa huwa na muongozo wa video inavyotakiwa kuwa pamoja na vitu ambavyo msanii anapaswa kuambatanisha wakati wa kutuma, ambavyo visipokamilika hawawezi kuicheza video hiyo.
“Kwa mfano unakuta wasanii ambao wameshatuma video nadhani wananielewa jinsi ambavyo ilivyo, wanakwambia kuna vipimo jinsi ya kupima na jinsi ya kusubmit video yako, kila Television ina utaratibu wake wa kupokea kazi za watu kwahiyo ukienda kinyume na utaratibu wake hawawezi kuchezwa hata kama umeitengeneza kwa hela nyingi lakini ukikiuka vigezo na masharti yao basi haiwezi kuchezwa. ”
Hit maker wa ‘Zigo’ ametolea mfano wake mwenyewe pamoja na video ya msanii anayechipukia Barakah Da Prince ambaye video yake ya ‘Siachani Nawe’ iliyofanyika Dar tena na kuongozwa na director Khalfani ambaye pia ni miongoni mwa madirector wapya, imeweza kupitishwa na kuchezwa Trace na MTV Base.
“kwahiyo haijalishi wala eti kuwa kuchezwa Channel O au kuchezwa MTV basi lazima ukashoot South Africa hapana, kwasababu hata video zangu zimeanza kuchezwa MTV sio kwamba nilianza kwenda South Africa, nilianza kushoot hapa hapa. Na kuna watu wengine ambao tunawasupport tunaona kama Barakah Da Prince kashoot hapa hapa Tanzania amejipanga amefata masharti na video inaendelea kuchezwa, na kuna watu wengine wameshoot kwa gharama nyingi video zao hazichezwi, Kwahiyo hiyo dhana ifutike.Tengeneza video kali ambayo hata mtu akiziba masikio anajua ni kitu gani kinaendelea kwenye video. Kwa mfano ‘Ojuelegba’ ile ya Wizkid, ukiiangalia ni cheap video sio kwamba ni video kali[…] kwahiyo la msingi ni kuwa watu tutengeneze tu video za kueleweka kali zina storyboard nzuri na madirector wawe na hizo details za kuangalia wakitaka kutuma.
Aliongeza,
“Na uzuri wa vituo vikubwa kama kazi yako nzuri itapigwa tu hata kama hawakujui, kwa mfano kama mi nimeanza kuchezwa Trace, mtu ambaye ndio alikuwa anayepiga Trace video yangu ile ya ‘Speak With Your Body’ nimekuja kuonana naye baada ya miaka kama minne, kwa hiyo haijalishi ukiwa una kazi nzuri tu inapigwa ilimradi ufate tu vigezo vyao. By the way unavyotuma video lazima utume video nzito sio unatuma video ya 280 Mb, wao wanatakaga 5 Gb, 2Gb huko.” alimaliza.
Home
»
Bongo star
» AY atoa elimu kwa wanaodhani kuwa ili video ichezwe TV kubwa za nje ni lazima kushoot SA au kutumia gharama kubwa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment