0
Huu unaweza ukawa ni mwaka mzuri kwa msanii wa R&B, Benard Paul a.k.a Ben Pol ambaye ameweka wazi habari nyingine njema kwa mashabiki wake, kuwa amchaguliwa kushiriki kwenye msimu mpya wa kipindi cha Coke studio Africa mwaka huu.
Hit maker wa ‘Sophia’, Ben Pol amesema kuwa ndoto aliyokuwa nayo ya kushiriki kwenye show ya Coke Studio Africa imetimia na kuufanya mwaka 2015 uzidi kuwa wa mafanikio kwake.

“Hii ni platform ambayo nilikuwa naiota, nilipata simu yao mapema mwaka huu kutoka Coke Studio, nikapewa maelekezo tukafanya mazungumzo kidogo nikatumiwa mkataba tukaupitia tukasaini, deal ikawa closed tukawa tunasubiri tu official announcement.”

Ben Pol ataungana na wasanii wengine kutoka nchi mbalimbali za Africa kwenye show hiyo inayotarajiwa kuanza hivi karibuni ukiwa ni msimu wa tatu.

Post a Comment

 
Top