0
Hatimaye Vanessa Mdee ametoa jibu la kile watu wengi walikuwa wakihitaji kusikia kutoka kwake kama bado ni mtangazaji wa Choice FM.
Kupitia mahojiano aliyofanya na kipindi cha Mambo Mseto cha Radio Citizen ya Kenya jana, Vanessa alisema kwa sasa si mtangazaji tena wa redio hiyo ili kuupa nafasi zaidi muziki.

“Nimesitisha kwa muda kazi ya utangazaji ili kupa muziki kipaumbele. Mimi ni msanii kwanza. I just do music,” Vanessa alimweleza mtangazaji wa kipindi hicho, Willy M Tuva.

“Kwa sababu ya kuwa na show nyingi nje ya Dar es Salaam na kushoot video nyingi katika nchi za nje, niliona ni kama nilikuwa nawakwaza mabosi wangu,” aliongeza.

Katika hatua nyingine Vanessa alisema ameshafanya kazi na wasanii wa Kenya Juliani, Sauti Sol na Victoria Kimani.

Post a Comment

 
Top