Kifuatacho kati ya Diamond na Nay wa Mitego ni video ya wimbo wao ‘Mapenzi au Pesa’.
Na ni waongozaji wawili wanaofikiriwa zaidi kupewa ‘tender’ hiyo.
“Kuna madirector wawili, kuna mmoja kutoka Nigeria tunafikiria Godfather, pia nyumbani kuna mmoja tunamfikiria lakini haswa ni hao wawili ili kufanya kitu kiende kuwa kikubwa zaidi,” Nay wa Mitego aliiambia Clouds FM.
“Nisiwe mnafiki ni Hanscana,” aliongeza Diamond.
“Yeah Kwa nyumbani tunamfikiria Hanscana, kwa nje tunamfikiria Godfather na jamaa mwingine anaitwa PK,” alisisitiza Nay wa Mitego.
Diamond amesema wamemfikiria Hanscana na sio waongozaji wengine kwakuwa anakubali uwezo wake.
“Tuongee ukweli [Hanscana] anafanya vizuri, unajua video kuna ubora fulani wa picha nahisi anaweza akaufanya. Story na nini kila mtu anaweza kushoot lakini ubora wa picha inavyokuwa inatoka nahisi ndio kitu ambacho tunakiangalia.”
“Tunahisi kama Hanscana kwa sasa hivi anafanya vizuri na sisi tunafanya biashara, hatufanyi tu ilimradi lakini tunaangalia wapi tunapata maslahi.”
Diamond aliongeza kuwa Hanscana pia ni muongozaji anayejituma na kufanya kazi haraka.
Home
»
Bongo star
» Hawa ndio waongozaji wanaofikiriwa kupewa kazi ya kushoot video ya ‘Mapenzi au Pesa’ ya Diamond na Nay
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment