0
Kuna usemi usemao kuwa ‘wagombanao ndio wapatanao’ na hiki ndicho kilichotokea weekend hii.

Diamond akiwa amevaa nguo ya Roperrope ambayo designer wake mmarekani alidai kuwa ni feki Devontae Roper, ni designer wa Los Angeles, California, Marekani ambaye ametokea kujipatia umaarufu kwa nguo zake zinazovaliwa na mastaa wa muziki nchini humo wakiwemo August Alsina, YG, Chris Brown, Future na wengine. Brand yake inajulikana kwa jina la RoperRope.


Devontae Roper

Juzi Roper alipost picha ya Diamond Platnumz akiwa amevaa nguo zenye mfanano na designs zake na kumchana staa huyo kuwa ameiba ubunifu wake kupitia yule Diamond aliyemuita kama ‘designer’ wake ambaye kazi yake hasa ni ‘stylist’.



“I usually don’t blast people who make or wear fakes of my designs but this person went way too far when they used my logo! @diamondplatnumz is wearing fake #Roperrope shirt made by a person with bad character and a strong lack or originality! This is not ok! If you steal a design please reframe from using the Designers Logo because it’s illegal www.shoproperrope.com,” aliandika kwenye Instagram.

Post hiyo ambayo hata hivyo tayari imefutwa ilisababisha mjadala mkubwa na wengi iliwafanya wamfahamu Roper ambaye nguo zake zimekuwa zikionekana kwenye video nyingi za August Alsina, Future na Chris Brown.

Wapo waliomshutumu Diamond na kudai kuwa ameumbuka lakini wengi walimtetea na kwa kusema yeye ni mvaaji tu wa nguo hizo na hana kosa hata kama alivaa nguo feki.

Mimi ni mmoja watu niliokuwa na mtazamo tofauti. Hii nipost niliyoweika Instagram kutoa ushauri wangu:

“Hili suala mimi nalionea katika muktadha chanya zaidi. Designer anayewavalisha August Alsina, Future, Meek Mill, Draya na wengine kamlalamikia Diamond kuvaa nguo feki zinazoiga brand yake. Naamini Diamond hana kosa kama lipo labda ni kumuita ‘stylist’ wake ‘designer’ na hivyo kuhisi Diamond anavaa nguo zake feki zilizotengenezwa na designer wa Diamond ambaye basically kazi yake ni kumchagulia bosi wake nguo za kuvaa. Binafsi mimi leo ndo nimemjua roperrope na nina uhakika wengi pia wamemjua leo thanks to Diamond. That means roper kapata exposure kubwa Tanzania na zaidi ya hapo. Diamond na roper wanaweza kufanya kitu pamoja. Hakuna shaka kuwa Diamond ni fan wa design zake na anaweza kumudu gharama za kupata customised outfits kutoka kwake na huenda akawa brand ambassador wake Mkubwa Afrika. Wanasema everything happens for a reason and I think this is not just a coincidence but something that was planned by a higher force (God). @diamondplatnumz make the most of this encounter and I bet you gonna be one of the best dressed African entertainers.”


Roper aliweka post ya pili kusisitiza kile alichokisema awali na kudai kuwa hakumuuzia Diamond nguo hizo. Hapo ndipo watu wengi waliifahamu vyema drama hiyo kiasi cha kuanza kuhisi kuwa designer huyo anatafuta umaarufu.

Kwenye post hiyo nilicomment tena kama ifuatavyo:



Huenda maneno yangu na ya wengine waliohisi wawili hawa wanaweza kuweka pembeni tofauti hiyo fupi na kufanya kazi yaliwaingia.

Roper alipost picha nyingine ya Diamond na kuandika: Bless Up emoji🏼 I just got news #Roperrope just went International emoji God is everywhere #YoungGod x #ICantLose #ShippingOverseas #ThanksEastAfrica #GodFlow @DiamondPlatnumz hit me up next time.”

Post a Comment

 
Top