0

Story kubwa tatu kwenye 255 ambayo imeruka kwenye show ya #XXL @CloudsFM

iko ya Mwana Hiphop Fareed Quincy Kubanda aka Fid Q, Mkali wa Rhymes kutoka Moro Town Afande Sele pamoja na mkali mwingine kwenye Chart ya Muziki Bongo, Bill Nas.

Kama umemuona Fid Q akifanya show na Live Band basi taarifa ikufikie kwamba jamaa kasema huu ndio utaratibu wake mpya kwenye muziki ambapo amesema hayo ni mabadiliko yake makubwa kuanzia sasa kwenye show zake.


Rapper Fid Q

Kama uliwahi kujua milioni ambazo Fid Q alikuwa akilipwa kwenye show yake ‘enzi za CD playback’, sasa hivi mambo yamebadilika pia.. malipo kwa show yameongezeka na tayari kapiga show mikoa mbalimbali TZ ikiwemo Dar ambako wameukubali sana ujio wake mpya. Kila la heri Fid Q !!

Afande Sele ni mmoja ya mastaa ambao wametangaza kugombea Ubunge kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu TZ.. Labda na wewe umewahi kuona Picha ambazo sio nzuri za staa huyo mitandaoni.. Afande amesema katika safari yake kuelekea Ubunge hivyo ni vikwazo vinavyoonesha mti mwema unapigwa mawe.


Msanii Afande Sele

Afande amesema kwamba kila ambae anasimama kumchafua yeye anaamini kwamba hiyo ni dalili kwamba anamuogopa au anamhofia jinsi ambavyo anakubalika na watu.

Malalamiko ni mengi kwenye headlines kuhusu #KTMA2015.. msanii Bill Nas amesema baadhi ya mastaa ambao walifanya muziki mzuri wakamshawishi na yeye kufanya muziki ni pamoja na Juma Nature, Jay Moe, Mr. Blue, Dully Sykes na wengineo ambao ni wakongwe lakini hawakuwahi kushinda Tuzo hizo.


Msanii Bill Nas

Bill anasema hata ikitokea ameshinda Tuzo 12 bado hawezi kujiona mkali kuzidi watu ambao walimvutia yeye kufanya muziki na bado hawakuwahi kupata Tuzo.

CHANZO XXL CLOUS FM:

Post a Comment

 
Top