0
Miss Tanzania 2001, Happiness Millen Magese ni staa pekee aliyetajwa kutunukiwa tuzo mpya ya BET mwaka huu iitwayo ‘Global Good Award’
Maana yake ni kuwa Millen atakabidhiwa tuzo hiyo siku ya utoaji wa tuzo hizo utakaofanyika June 30.

Millen ametajwa kwenye kipengele hicho kutokana na jitihada zake za kampeni ya ugonjwa wa endometriosis ambao pia amekuwa nao katika maisha yake yote tangu awe msichana. Tatizo hilo limempelekea kuwa mgumba.

Pamoja na hivyo Millen amekuwa mstari wa mbele kutoa misaada mbalimbali kwa wasiojiweza.

Hivi karibuni mpenzi wa staa wa Nigeria, Wizkid aitwaye Tania Omotayo alimfisia Millen kwenye Instagram kwa anavyojitolea.

“Words are not enough to explain how amazing this woman is!!! Thank you so much for being there for me!!! You are a very rare gem!!! God will bless you for me my love @ladivamillen we will win… #WCW #Superwoman,” aliandika Tania.

Post a Comment

 
Top