“Miaka itaenda miaka itarudi wasanii watakuja wasanii wataondoka hakika hawezi kutokea tena Prof Jay mwingine wala wa kufanana naye,” alisema Kala.
“Heshima yake itabaki milele. Alivyowahi kuvifanya sio vya kawaida amefanya kazi kubwa sana. Kwanza alibadilisha muziki na kuufanya kukubalika kwa watu wote. Akaondoa ile dhana ya usanii ni uhuni.”
“Lakini pia akatunga tungo za kumshawishi kila mtu kukubali atake asitake. Na sasa imani yangu kwake kwenye suala lake la kugombea ubunge Mikumi ni kubwa sana naamini yale mapinduzi aliyoyaleta kwenye muziki atayaleta pia bungeni.”
Post a Comment